Hekaheka part II: kilichoendelea baada ya watu kumvamia mzee aliyedaiwa kujeruhi watu kwa bastola
- posted by salum.
- May 20, 2015
- 1 min read
Jana kulikuwa na Hekaheka kutoka Kurasini Dar iliyokuwa inahusu ishu ya mzee moja kudaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wawili, baadae wakavamia watu ambao walifanya vurugu na kuchoma moto gari la mzee huyo alafu wakawa wanataka kuchoma moto na nyumba yamzee huyo pia....
Mashuhuda waliongea jana, tuhuma na lawama zao walizipeleka kwa mzee huyo kwamba ni kawaida yake kuwatishia bastola watu wanaopita jirani na nyumba yake au wanaompigia kelele.
Leo kasikika mtoto wa mzee huyo ambae amesimulia hali ilivyokuwa kuanzia mwanzo mpaka mwisho.. mtoto huyo amesema kuwa baada ya baba yake kuokolewa na Polisi watu hao walivamia tena nyumba hiyo wakamjeruhi mtu mmoja ambae aliachwa na Polisi kwa ajili ya kulinda.. wao walikuwa kwenye uvungu wa kitanda pamoja na ndugu zake wengine wakati ishu yote inatokea.
Mtoto huyo amesema nao pia walivamiwa na kundi la watu, wakawa wanatishia kuwanyang’anya simu na hela, baadae nao wakaja kuwaokoa, wakatoa na vitu vingine vyote kwenye nyumba.

Comments